Karen Christence Blixen-Finecke (jina la kiuandishi alilotumia kwenye nchi zinazozungumza Kiingereza: Isak Dinesen) (Rungsted/ Denmark17 Aprili1885 - 7 Septemba1962) alikuwa mwandishi kutoka nchi ya Denmark. Alitumia pia majina ya Tania Blixen, kwenye nchi zinazozungumza Kijerumani, Osceola na Pierre Andrézel.
Aliandika kumbukumbu ya maisha yake Kenya na kitabu hiki kikawa msingi wa filamu "Out of Africa". Huko Denmark alijulikana sana kwa kazi yake iitwayo Seven Gothic Tales.
Early years
Karen Dinesen alizaliwa Rungstedlund, kaskazini mwa Copenhagen. Baba yake, Wilhelm Dinesen (1845–1895), alikuwa ni mwandishi na ofisa wa kijeshi toka familia ya wamiliki wa mashamba ya Jutland yenye uhusiano wa karibu na ufalme, kanisa na siasa za mrengo wa kulia. Mama yake, Ingeborg Westenholz (1856–1939), alitoka kwenye familia tajiri inayofanya biashara. Karen Dinesen alikuwa ni mtoto wa pili kati ya watoto watatu wa kike na wawili wa kiume. Mdodo wake wa kiume, Thomas Dinesen, alipata tuzo ya Victoria Cross wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Dinesen was known to her friends as "Tanne".
Vitabu
Eneboerne (The Hermits), Agosti 1907, kilichapishwa kwa jina la Tilskueren kwa jina lake la uandishi Osceola
Pløjeren (The Ploughman), Oktoba 1907, kwa jina la Gads danske Magasin,akitumia jina la Osceola
Familien de Cats (The de Cats Family), Januari 1909, kwa jina la Tilskueren akitumia jina la Osceola
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Karen Blixen kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.