Juliana wa Nikomedia (Nikomedia, leo Izmit nchini Uturuki, 286 hivi - 304 hivi) alikuwa bikira Mkristo aliyefia dini yake kwa kukatwa kichwa katika dhuluma ya kaisari Diocletian akiwa na umri wa miaka 18 hivi alipokataa kuolewa na mtawala Mpagani.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 16 Februari au 21 Desemba (kwa Waorthodoksi).
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |