Madini silikati ni madini yanayounda miamba mbalimbali. Yote yanaundwa na anioni zenye silikoni na oksijeni. Ndilo kundi kubwa na muhimu zaidi katika madini yote likifanya karibu asilimia 90 za ganda la Dunia.
Silika (dioksidi ya silikoni) SiO2 kawaida huhesabiwa kuwa madini silikati. Silika hupatikana katika maumbile kama shondo na maumbo yake.
Madini silikati kimsingi ni kampaundi ya ioni ilhali anioni zake huwa na atomi za silikoni na atomi za oksijeni.
Katika madini mengi kila atomi ya silikoni iko katikati ya kitovu cha piramidi pembetatu (tetrahedron), ambako pembe zake ni atomi za oksijeni nne.
Kikundi kikuu | Muundo | Fomula | Mfano |
---|---|---|---|
Nesosilikati | pekee ya silicon tetrahedra | 4− | olivine |
Sorosilikati | tetrahedra mara mbili | 6− | epidote, kikundi cha melilite |
Saiklosilikati | pete | 2 n - | kikundi cha tourmaline |
Inosilikati | mnyororo mmoja | 2 n - | kikundi cha pyroxene |
Inosilikati | mnyororo mara mbili | 6 n - | kikundi cha amphibole |
Filosilikati | shuka | 2 n - | mica na clay |
Tektosilikati | Mfumo wa 3D | x - | shondo, feldspars, zeolites |
|archivedate=, |accessdate=
(help)
Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Madini silikati kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |