Nadharia ya njama(kwa Kiingereza: conspiration theory) ni masimulizi yanayodai kwamba kundi la watu ("wala njama") wamepatana kwa siri ("kula njama") kufanya mambo haramu au mabaya na kuyaficha mbele ya umma.
Nadharia za njama kwa kawaida zina ushahidi mdogo au zinakosa ushahidi wowote. Kuna pia nadharia za njama zinazorejelea matukio halisi lakini kuzieleza kutokana na njama isiyojulikana na watu wengi.
Nadharia nyingi za njama zinadai kwamba matukio fulani ya kihistoria hayakutokea jinsi yanavyoelezwa katika vitabu vya historia bali kufuatana na njama fulani.
Mifano
Nadharia za njama zilizokuwa maarufu katika miaka iliyopita ni pamoja na
kwamba kutua mwezini kwa Apollo 11 hakukutokea, picha zote zilipigwa duniani tu