Servatius wa Tongeren (kwa Kiarmenia: Սուրբ Սերվատիոս; kwa Kiholanzi: Sint Servaas; kwa Kifaransa: Saint Servais; alizaliwa nchini Armenia, akafariki Maastricht, 384) alikuwa askofu wa kwanza wa Atuatuca Tungrorum, leo Tongeren, nchini Uholanzi.
Katika mitaguso mbalimbali alitetea imani sahihi ya Mtaguso wa kwanza wa Nisea dhidi ya uzushi wa Ario kuhusu Yesu Kristo.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 13 Mei.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |