Zuonosia (kutoka Kiingereza: zoonosis, zoonotic desease) ni ugonjwa wa kuambukiza wenye asili ya mnyama unaosababisha ugonjwa wa binadamu.
Magonjwa ya zuonosia huenea kwa njia ya bakteria, virusi, fungi au vimelea.
Magonjwa hayo hutokea mara nyingi. Imekadidiriwa kuwa mnamo asilimia 60 za magonjwa ya kuambukiza yote ni ya zuonosia, yaani maambukizo hupitia wanyama au wadudu.
Maambukizi hutokea kiasili hasa kwa njia mbili
Magonjwa mengi yanayotokana na chakula ni magonjwa ya zuonosia. Hapo mwanadamu anagonjeka kutokana na kula kitu ambacho kilitoka kwa mnyama mgonjwa.
Viambukizi vya kawaida ambavyo husababisha magonjwa kupitia chakula ni bakteria wa salmonella, campylobacter, na escherichia coli (E. coli). Mayai, samaki, nyama ya kuku, na maziwa vinaweza kubeba bakteria hao na kusababisha magonjwa yanayotokana na chakula, kama usumisho wa chakula, kwa wanadamu.
Magonjwa ya zuonosia yanayoambukizwa kupitia chakula ni pamoja na:
Ugonjwa | Pathojeni (kiambukizi) |
---|---|
Bruselosisi | bakteria ya brucella |
Kipindupindu | bakteria ya kipindupindu |
ugonjwa wa Creutzfeldt-Jakob | prioni |
listeriosisi | bakteria ya Listeria |
toksoplasmosisi | vimelea vya toxoplasma gondii |
Mara nyingi, watu wanaweza kuzuia maabukizi kupitia chakula kwa kukipika kwa muda wa kutosha na hivyo kuua bakteria au vimelea vilivyomo.
Yafuatayo ni mifano ya magonjwa ya zuonosia ambayo wanadamu wanaweza kuambukizwa moja kwa moja kutoka kwa wanyama wagonjwa walio hai.
Ugonjwa | Pathojeni (kiambukizi) |
---|---|
kimeta (anthrax) | bakteria ya bacillus anthracis |
homa ya mafua (influenza) | virusi vya influenza A |
homa ya Lassa | virusi vya lassa |
kichaa cha mbwa | virusi vya rabies |
toksoplasmosisi | vimelea vya toxoplasma gondii |
kifua kikuu | bakteria ya mycobacterium bovis |
Ugonjwa | Pathojeni | Kimelewa (mwenyeji) | Vekta | |
---|---|---|---|---|
ugonjwa wa malale | vimelea vya trypanosoma brucei rhodesiense | Wanyama mwitu na wa kufugwa mbaimbali | mbung'o | |
tauni (bubonic plague) | bakteria ya yersinia pestis | panya, rodentia | viroboto | |
homa ya dengi | virusi vya dengue (flavi) | binadamu na nyani | mbu wa aedes | |
borrelosia (borreliosis, Lyme desease) | bakteria ya borrellia | mamalia na ndege | papasi | |
malaria | vimelea vya plasmodium | binadamu | mbu, hasa anopheles | |
homa ya Naili magharibi (West Nile fever) | virusi vya Naili magharibi (West Nile virus) | hasa ndege | mbu |
Kuna virusi mbalimbali ambavyo kwa kawaida vinapatikana kwa wanyama vinavyoweza kubadili tabia kadhaa na kupata uwezo wa kuathiri binadamu.
Mabadiliko ya aina hiyo yametazamwa hasa kwa virusi vya influenza vya ndege, nguruwe na farasi, halafu kwa virusi vya corona.
Wakati virusi vya wanyama vinapata uwezo wa kusambaa kutoka mtu hadi mtu, vinaweza kuathiri watu wengi kwa sababu ni "virusi vipya". Maana mwili hupambana na virusi kwa uwezo wa mfumo wa kingamaradhi (immune system) unaochungulia virusi na kutoa zindikomwili (antibodi) zenye uwezo wa kuzuia virusi. Mfumo wa kingamaradhi hukumbuka mashambulio ya miaka ya nyuma, lakini virusi vipya ni changamoto kwa mfumo huo. Kama virusi vipya kutoka mnyama fulani ni tofauti sana na vyote vilivyotangulia uwezo wake wa kusababisha hatari kali ya afya ni mkubwa. Hapa kuna uwezekano wa mlipuko wa maambukizi (epidemia, hata pandemia) jinsi ilivyotokea kwenye tauni ya karne za kati, na influenza ya 1918.
|date=, |accessdate=
(help)
|date=, |accessdate=
(help)
|date=, |accessdate=
(help)
|accessdate=
(help)
|date=
(help)
|accessdate=
(help)
|date=, |accessdate=
(help)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Zuonosia kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |