Paliumu (kutoka Kilatini pallium) ni vazi linalotumika katika Kanisa la Kilatini.
Kwanza lilitumiwa na Papa wa Roma tu, lakini baadaye lilianza kutolewa naye kwa maaskofu wakuu kuonyesha mamlaka waliyonayo juu ya maaskofu kwa kushirikishwa na Ukulu mtakatifu.
Vazi lenyewe ni utepe mweupe uliotengenezwa kwa sufu ya mwanakondoo na uliotiwa misalaba myeusi sita: mine katika duara na miwili katika sehemu inayoangukia kifuani na mgongoni.
Utepe huo unavaliwa shingoni wakati wa adhimisho la Misa katika jimbo kuu na majimbo ya kanda yake, ila Papa anauvaa duniani kote kuonyesha hadhi yake kama mchungaji mkuu wa kundi lote la Kristo kadiri ya imani ya Kanisa Katoliki.
Maaskofu wa Ukristo wa Mashariki huwa wanavaa nguo inayofanana, lakini ni pana zaidi: omofori.
|accessdate=
(help)|date=, |accessdate=
(help)|date=
(help)|date=
(help)—a monograph published by the Archdiocese of Cardiff to mark the bestowal of the Pallium on Archbishop George Stack in July 2011.|date=
(help)Makala hii kuhusu Kanisa Katoliki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Paliumu kama historia yake au maelezo zaidi? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |