"Mwana wa Mungu" ni jina linalotumiwa katika dini mbalimbali ili kusisitiza uhusiano wa mtu fulani na Mungu au mmojawapo wa miungu. Kwa maana hiyo lilitumika hasa kwa ajili ya watawala.
Pengine linamaanisha viumbe vingine, kama vile malaika.
Kadiri ya Injili, Yesu Kristo mwenyewe alisisitiza mara nyingi uhusiano wake wa pekee na Baba wa mbinguni kutokana na asili yake toka juu, tofauti na ile ya watu wengine wote.
Mtaguso huo ulitunga kanuni ya imani iliyokiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu kwa maana ana hali moja na Mungu Baba, hakuumbwa bali alizaliwa naye tangu milele yote.
Wakristo wanapomkiri Yesu kuwa Mwana pekee wa Mungu maana yake ni kwamba, kabla hajazaliwa kama mtu duniani ni Mungu, sawa na Baba anayemzaa yeye tu tangu milele. “Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu… Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu… Amwaminiye yeye hahukumiwi, asiyemwamini amekwisha kuhukumiwa; kwa sababu hakuliamini jina la Mwana pekee wa Mungu” (Yoh 1:1,14; 3:18).
Msimamo wa Uislamu
Uislamu unamheshimu Yesu kama nabii mmojawapo, lakini unakanusha kabisa jina hilo na maana yake yoyote ili kusisitiza upekee wa Mungu.
Pelikan, Jaroslav. Development of Christian Doctrine: Some Historical Prolegomena. London: Yale University Press. 1969.
_______ The Emergence of the Catholic Tradition (100-600). Chicago: University of Chicago Press. 1971.
Schweitzer, Albert. Quest of the Historical Jesus: A Critical Study of the Progress from Reimarus to Wrede. trans. by W. Montgomery. London: A & C Black. 1931.
Tyson, John R. Invitation to Christian Spirituality: An Ecumenical Anthology. New York: Oxford University Press. 1999.
Wilson, R. Mcl. Gnosis and the New Testament. Philadelphia: Fortress Press. 1968.
Witherington, Ben III. The Jesus Quest: The Third Search for the Jew of Nazareth. Downers Grove: InterVarsity Press. 1995.
_______ “The Gospel of John.” in The Dictionary of Jesus and the Gospels. ed. by Joel Greene, Scot McKnight and I. Howard
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mwana wa Mungu kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.