Seva mbadala (kwa Kiingereza: proxy server) ni seva ambayo inapatanisha ombi la wateja wa mtandao kwa seva nyingine. Kwa ufupi, huwa katikati na kazi yake ni kupatanisha wateja na wanachokihitaji.
Seva mbadala zilitengenezwa ili kuleta muundo mwafaka katika mifumo iliyosambazwa ya kompyuta (distributed computer systems). Leo hutumika sana kwa mitandao ili kuficha anwani ya IP ya mteja.
Inafaa uchague seva mbadala ambayo ina kasi nzuri hivi kwamba inaweza kuwahudumia wateja wako kwa kasi nzuri wasije kuona kana kwamba mambo yatendeka polepole.
Seva mbadala yako iwe na nafasi kubwa ya kuhifadhi yale yote yaliyoko kwa seva na mitandao yako yote.
Seva yako lazima iwe ni salama isije ikaingiwa na kuibiwa manenosiri na hackers.
Ni vyema seva mbadala iwe mahala ambapo wateja watafikia huduma kwa urahisi yaani iwe karibu na nchi walioko.
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |